Klabu yetu imefanikiwa kumsajili mshambuliaji Moses Phiri raia wa Zambia aliyekuwa anachezea Zanaco FC ya nchini humo kwa mkataba wa miaka miwili.

Phiri ambaye pia anaweza kucheza nafasi za kiungo mshambuliaji na winga zote mbili atavaa jezi nyekundu na nyeupe kuanzia msimu ujao wa mashindano.

Phiri ni usajili wetu wa kwanza kuelekea maboresho  makubwa ya kikosi chetu ambayo tumepanga kuyafanya kuelekea msimu mpya unaotarajiwa kuanza mapema hivi karibuni.

Msimu uliopita akiwa na Zanaco Phiri amefunga mabao 14 kwenye ligi kuu ya Zambia akiwa ni mfungaji bora namba mbili nyuma ya kinara mwenye mabao 16

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.