Home
Unlabelled
SIMBA YA SELEMAN MATOLA INAOGOPESHA
SELEMAN Matola, Kaimu Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba ameweza kuifanya timu hiyo kuweza kuogopesha kwenye mechi tatu ambazo amekaa kwenye benchi.
Matola amekaimu mikoba ya Pablo Franco ambaye alikuwa kocha mkuu kabla ya kufutwa kazi kutokana na kushindwa kufikia makubaliano ambayo alipewa na mabosi hao ikiwa I pamoja na kukosa ubingwa wa ligi na Kombe la Shirikisho.
Mchezo wa kwanza Matola aliongoza ilikuwa mbele ya Mbeya City na Simba ilishinda mabao 3-0 na mchezo wa pili ilikuwa Simba 3-1 KMC na ule wa tatu ilikuwa Simba 2-0 Mtibwa Sugar.
Kwenye msako wa pointi 9, Matola kasepa nazo zote huku safu yake ya ushambuliaji ikitupia mabao 8 na kuruhusu bao moja la kufungwa kwenye upande wa ulinzi na timu hiyo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 60 baada ya kucheza mechi 28.
Matola amesema kuwa yote hayo wamekuwa wakiyafanyia kazi kwenye eneo la uwanja wa mazoezi.
“Ushindani ni mkubwa na wachezaji wanafanya kile ambacho tunawaelekeza hivyo ninawapongeza wachezaji kwa kuwa wamekuwa wakifanya vizuri na sapoti kutoka kwa mashabiki imekuwa kubwa,” .
Leo Simba inatarajia kumenyana na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi Uwanja wa Sokoine, Mbeya
Post a Comment