Kaimu Kocha Mkuu Seleman Matola, ameweka wazi kuwa lengo letu lililobaki ni kuhakikisha tunamaliza ligi kwa heshima baada ya kuwa na nafasi ndogo ya kutetea ubingwa msimu huu.

Matola amesema tunahitaji kushinda mechi zote tano zilizobaki kwa ajili ya kuweka heshima na kuwapa furaha mashabiki.

Matola amesema maandalizi kuelekea mchezo wetu dhidi ya Mbeya City yanaendelea vizuri baada ya wachezaji waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa wamerejea na wamefanya mazoezi na wenzao.

Matola ameongeza kuwa wachezaji Medie Kagere na Peter Banda ndiyo pekee ambao hawajarudi lakini wanataraji kutua nchini muda wowote kuanzia sasa.

“Hatuna nafasi ya kutetea ubingwa lakini tunataka kuweka heshima kwa kushinda mechi zote tano zilizobaki ili kuwapa furaha mashabiki wetu,” amesema Matola.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.