MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi ameunga mkono mfumo wa Klabu Maarufu ya Mchezo wa soka ya Yanga kuanzisha miradi ya kujitegemea katika azma ya kuiondoshea na utegemezi Klabu hiyo.

Balozi Seif Ali Iddi ameyasema hayo ofisini kwake Vuga-Zanzibar wakati akizungumza na Uongozi wa Yanga.

Balozi Seif amesema kwa kuwa Klabu hiyo ina dhamira sahihi ya kuendeleza Wachezaji wake katika azma njema ya kuimarisha ustawi wao yeye binafsi pamoja na Serikali iko tayari kusaidia nguvu zake ili kuona malengo iliyojipangia yanafanikiwa vizuri.


 Mwenyekiti wa Yanga Dr. Mshindo Msolla amemueleza Balozi Seif kwamba uongozi umelenga kuyasimamia mambo matano makubwa yatakayosaidia kuipeleka klabu hiyo katika mafanikio.

Mambo hayo ni pamoja na kuleta umoja katika kuipeleka timu kwa wanachama, kuimarisha Miradi iliyopo klabuni na kubuni mengine mipya, uwajibikaji na utawala bora pamoja na kuiendeleza miradi iliyopo Visiwani Zanzibar.

Amesema katika mfumo huo Mpya utakaoanzishwa, Wanachama watakuwa na uwezo wa kujua mapato na matumizi ya klabu kupitia mtandao wa kisasa wa Habari na Mawasiliano utakaokwenda sambamba na kuongeza Wanachama kutoka 17,000 hadi kufikia Milioni 1,000,000.
Tags:
Newer Post
This is the last post.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.