July 2019


SALIM Aiyee. mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' amesema kuwa wana imani ya kupata matokeo mbele ya Kenya kwenye mchezo wa marudio.

Stars ina kibarua cha kutafuta matokeo chanya kwenye mchezo wa marudio utakachezwa Kenya Agosti 4 baada ya mchezo wa kwanza kulazimisha sare ya bila kufungana.

Aiyee amesema kuwa:"Ushindani utakuwa mkubwa ila kutokana na mazoezi pamoja na mbinu mpya kutoka kwa benchi la ufundi tunaamini tunakwenda kufanya vizuri.

"Bado tuna nafasi ya kupata matokeo ugenini kwani mchezo wa mpira ni dakika tisini hivyo tunakwenda kupambana,mashabiki waenelee kutupa sapoti" amesema.


CLIFFORD Ndimbo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema kuwa leo ndio mwisho wa usajili kwa wachezaji wa ndani.

 Ndimbo amesema kuwa hakuna muda mwingine wa nyongeza kwa wale ambao bado hawajakamilisha zoezi.

"Julai 31 zoezi la usajili linafungwa jumla na hakuna muda wa kuongeza kwa wale ambao hawajakamilisha usajili.

"Timu nyingi zinakamilisha usajili wa ndani pekee na kusahau kuwasajili wachezaji hao kwa njia ya mtandao yaani TFF Connect, hilo wasilisahau ni lazima wafanye hivyo" amesema.

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limechagua waamuzi kutoka nchini Sudan kuchezesha nchezo wa raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Azam FC na Fasil Kenema ya Ethiopia.

Mchezo huo wa kwanza wa Azam FC unatarajiwa kuchezwa  Uwanja wa Taifa wa Bahir, Agosti 11 mwaka huu mjini Bahir, Ethiopia majira ya saa 10.00 jioni.

Mwamuzi wa kati wa mchezo huo, anatarajia kuwa Elsiddig Mohamed Eltreefe, mwamuzi msaidizi namba moja akiwa, Elmoiz Ali Mohamed Ahmed na namba mbili akisimama Haitham Elnour Ahmed huku Sabri Mohamed Fadul akiwa mwamuzi wa akiba.

Kamishna atayesimamia mchezo huo anatarajia kutokea kwenye visiwa vya Reunion, ambaye ni Ismael Locate.

MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ameona namna wachezaji wake wanavyocheza na kujituma hivyo ana imani msimu ujao watakuwa juu zaidi ya msimu uliopita.

Zahera yupo na timu mkoani Morogoro ikiwa imeweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao amesema kuwa ameridhishwa na uwezo wa wachezaji wake wote.

Akizungumza na Saleh Jembe, Zahera amesema kuwa:-"Kuhusu aina ya wachezaji wangu nimewaona kwa ukaribu kuanzia kwenye mechi yao iliyopita na hata mazoezini wote wapo vizuri.

"Wachezaji wangu wana uwezo wa kumiliki mpira na kutoa pasi kwa wakati hivyo msimu ujao tutakuwa juu zaidi ya msimu uliopita," amesema.

Miongoni mwa wachezaji wapya ambao wamesajiliwa msimu huu ndani ya Yanga ni pamoja na Ally Ally, Juma Balinya, Patrick Sibomana, Mapinduzi Balama.


KIKOSI cha Simba leo kinacheza mchezo wake wa mwisho wa kirafiki wa kufunga hesabu dhidi ya Orlando Pirates nchini Afrika Kusini.

Mchezo huo ambao ni maalumu kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao utachezwa majira ya jioni kabla ya kesho kuanza safari kurejea Dar.

Leo kikosi kilisafiri kutoka ilipo kambi yao maeneo ya Rustenburg mpaka Johannesburg sehemu watakayocheza leo.

Patrick Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema lengo kubwa la michezo hiyo ni kuunda muunganiko bora kwa ajili ya msimu ujao.

Sadney Urknob leo amekiwasha kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Friends Ranger uliochezwa uwanja wa Highland Park kwa kufunga moja ya bao kwenye ushindi wa mabao 2-0.

Leo Yanga ilicheza mchezo wa kirafiki kwa lengo la kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao wakiwa chini ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera.

Sadney alipachika bao hilo dakika ya 38 na bao la pili lilifungwa na Papy Tshishimbi dakika ya 64.

CRESCENTIUS Magori, Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba amesema kuwa jeshi kamili la Simba linatarajiwa kurejea kesho kutoka Afrika Kusini kwa ajili ya maadalizi ya mwisho ya mchezo wao wa kirafiki pamoja na ule wa kimataifa.

Kikosi cha Simba kimeweka kambi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Bara pamoja na michuano ya kimataifa.

Magori amesema:"Kikosi kitarejea Julai 31 kutoka kambini nchini Afrika baada ya kumaliza ratiba ya maandalizi ya michuano ya kimataifa pamoja na Ligi Kuu Bara.

"Wanarejea kwa ajili ya kazi moja kuendeleza moto wa Simba kuelekea Simba day na maandalizi ya mwisho kwenye mchezo wetu wa kirafiki dhidi ya Power Dynamo, na ule wa kimataifa dhidi ya UD Songo" amesema.

ANWAR Binde, Ofisa Habari wa klabu ya KMC amesema kuwa kwa sasa vijana wanazidi kutengamaa kuelekea mchezo wao wa kimataifa dhidi ya AS Kigali.

KMC itamenyana na AS Kigali, Agosti 10 nchini Kigali ukiwa ni mchezo wa awali kwenye michuano ya kombe la Shirikisho.

Akizungumza na Saleh Jembe, Binde amesema kuwa mazoezi wanayoyafanya wachezaji wao yanawaimarsha kila siku.

"Kwa sasa tupo kwenye maandalizi kuelekea kwenye michuano ya kimataifa na vijana wanaonyesha utofauti kila iitwapo leo.

"Dozi ya asubuhi na jioni wanayoipata pale Uwanja wa Bora inawajenga hivyo matumaini makubwa ni kufanya vema kwenye mchezo wetu huo," amesema.


ETTINE Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili ya michuano ya kimataifa pamoja na Ligi Kuu Bara.

Azam FC itamenyana na Fasil Kenema kwenye mchezo wa kwanza wa Shirikisho utakaochezwa Agosti 10 nchini Ethiopia.

"Tunajua tuna kazi kubwa kwenye michuano ya kimataifa pamoja na ligi, kwa sasa tumeanza kujiaanda na michuano ya kimataifa na tupo tayari kwa ushindani," amesema.

 Zimebaki siku 12 kabla ya Azam FC ambao ni mabingwa wa kombe la Shirikisho kuvaana na Fasil Kenema ya Ethiopia.


DANIELE Rugan yupo kwenye hesabu za kusajiliwa na klabu ya Arsenal kwa mkopo akitokea ndani ya kikosi cha Juventus.


Beki huyo msimu uliopita akiwa na Juventus amecheza jumla ya mechi 20 kwenye mashindano yote ya Juventus.

Kwa sasa thamani yake inatajwa kuwa pauni milioni 40 na Meneja wa Arsenal, Unai Emery anaamini atakuwa msaada ndani ya kikosi hicho cha washika bunduki.


Rugani nafasi yake ni finyu kikosi cha kwanza kutokana na Juventus iliyo chini ya Maurizio Sarri kumsajili kinda Matthijs de Ligt kutoka Ajax.


JUMA Mwambusi, Kocha Mkuu wa Mbeya City amesema kuwa kazi kubwa wanayo msimu ujao kwa kuwa hesabu zao ni kufanya vema.

Mwambusi amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya msimu pya na maandalizi yapo vizuri.

"Kwa sasa kila kitu kinakwenda sawa na wachezaji wapo tayari kwa msimu mpya, mashabiki wazidi kutupa sapoti," amesema.

Mchezo wa kwanza kwa Mbeya City utakuwa dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Agosti 24 uwanja wa Sokoine.

OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa hawana hofu na mchezo wao watakaocheza jumanne siku ya Simba day mashabiki wa Simba wanajua wanachokitaka.

Agosti sita Simba itacheza uwanja wa Taifa na timu ya Power Dynamo mchezo wa kirafiki wenye lengo la kuwatambulisha wachezaji wake wapya na wale wa muda mrefu.

"Haijalishi itakuwa ni jumanne watu wanasema hawatakuja watu sisi tunajua kwamba wana Simba wanapenda kuiona timu yao hivyo nawaomba wanasimba wanunue tiketi mapema ili kupunguza ule msongamano wa kujazana siku ya mwisho.

"Tumejipanga tunajua kwamba watu wanataka kumuona Kahata, wale Wabrazili pia wote watakuwwepo bila kumsahau Meddie Kagere, na wachezaji wengine wote, ni wakati wetu wa kutamba sasa," amesema.

CRESCENTIUS Magori, Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba amesema kuwa ratiba ya michuano ya kimataifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) imesababisha wapangue ratiba zao zote.

Magori amesema kuwa mwaka huu wamebadili ratiba  ya maadhimisho ya Simba day kutokana na ratiba kubana,kwani mechi yao ya kwanza kimataifa dhidi ya UD Songo itakuwa Agost 10.

"Tumeamua kubadili ratiba zetu zote baada ya Caf kutoa ratiba za awali, tumerudisha tarehe ya mechi nyuma mpaka sita tulipanga iwe tarehe 3 ambayo ni wikend ila  kuna wachezaji wetu wapo timu ya Taifa hivyo hatuwezi kufanya jambo lolote.

"Ratiba ya michuano kubadilika imetufanya tubadili ratiba kwani tulipanga kucheza Dar, Mwanza ila sasa mambo yamekuwa magumu hatuna nafasi, labda mwakani tunaweza kufanya hivyo.

"Tamasha hili lipo kwenye mipango na vyanzo vya Simba hivyo wakati mwingine itakuwa ni kubwa kuliko sasa na bajeti yake itakuwa kubwa na mipango inazidi kuiva na tunaifanyia kazi," amesema.

Agosti 6 Simba itacheza na Power Dyanamo kwenye kilele cha Simba day ambayo huwa maalumu kwa ajili ya kutambulisha jezi mpya pamoja na wachezaji wa Simba.


JULAI 31 dirisha la usajili kwa wachezaji wa ndani wa Ligi Kuu Bara linafungwa, Yanga bado wapo sokoni kutafuta nyota wakali wawili wa kujiunga na kikosi hicho.

Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa mpango uliopo ni kuweka nafasi zaidi ya mbili kwa kila mchezaji ndani ya Yanga ambayo inashiriki michuano ya kimataifa.

“Bado dirisha la usajili halijafungwa nasi tumebakiza nafasi mbili ambazo tunazifanyia kazi, hivyo muda wowote tunashusha mashine mpya,” amesema.

Inaelezwa kuwa wachezaji ambao kwa sasa wanasakwa ni mabeki engo likiwa kuchukua nafasi ya Juma Abdul na Andrew Vincent ambao inaelezwa wana dai stahiki zao.


EMMANUEL Amunnike habari zake kwa sasa zimeshafungwa kwa kuwa amekubaliana na hali halisi ya kukiacha kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania.

Matarajio ya wengi ilikuwa ni kwenye michuano ya Afcon kufanya vema na mwisho wa siku kila kitu kikawa tofauti na vile ambavyo wengi walikuwa wanaamini.

Ni jambo jema hasa kwa kuwa hakuna mgogogro wowote na pande zote mbili zimekubalina hasa ukizingatia kwamba watanzania wengi wanapenda kuona matokeo chanya hata TFF nao hesabu zao ni kuona Taifa linapata matokeo chanya.

Rekodi ambayo ameiweka itabaki kwenye kumbukumbu kwani licha ya kutimuliwa ni yeye ameiongoza timu kutinga hatua ya makundi ya michuano mikubwa Afrika ya Afcon akiwa ni Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania.

Hii imewezekana baada ya kupita miaka 39 ambayo wachezaji wote wanaoitumikia kwa sasa timu ya Taifa hakuna hata mchezaji mmoja aliyekuwa anakipiga ndani ya kikosi cha timu ya Taifa kwa wakati huo hivyo inamaanisha kwamba ni muda mrefu umepita.

Mema aliyoyafanya tutayakumbuka na hata maumivu ya kupoteza kwenye michuano yetu ya Afcon haitafutika kwani ni rekodi na hatuwezi kukataa kwamba mechi zetu tatu zote tulifungwa na tulimaliza kundi C tukiwa hatuna hata pointi moja zaidi ya kubeba furushi la mabao nane nasi tukifunga mabao mawili.

Ni rekodi yenye maumivu na uchungu hivyo inatoa taswirwa kwamba wakati ujao TFF ambao ndio wanaochagua kocha wa kuinoa timu ya Taifa wanatakiwa kuwa makini na kusimamia weledi wa kazi na sio kuweka mapenzi yao binafsi kwenye maslahi makubwa ya nchi.

Tukumbuke kuwa kwa sasa timu ya Taifa ipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu Ettiene  Ndayiragije akipeana sapoti na wazawa, Suleman Matola na Juma Mgunda na mchakato uliopo kwa sasa ni kufuzu michuano ya Chan.

Ukiachana na Chan bado tunahitaji kuwa na kocha mkuu wa timu ya Taifa ambaye atasuka kikosi kipya cha ushindani kwa ajili ya kufuzu pia michuano ya Afcon.

Hivyo bado kuna uhitaji wa kumpata kocha mwenye uwezo na mwenye kiu ya mafanikio pale ambapo anakuwa anafanya kazi na sio ilimradi tu.

Nasema hivyo kwa sababu ya yale ambayo yamejitokeza kwa Amunike alikuwa ni mpole wa sura ila mengi nyuma ya pazia wanayajua wachezaji wenyewe licha ya kutokusema hata TFF nao wanajua namna alivyokuwa.

Mwalimu wa aina hii kama atapewa nafasi tena basi kuyafikia mafanikio ya soka itakuwa ni historia hivyo kwa hili TFF liwe darasa na maamuzi yao yawe yenye manufaa kwa Taifa.

Ukubwa wa timu ya Taifa uendane na ukubwa wa mwalimu atakayekuja kuifundisha timu, vigezo muhimu vizingatiwe kwa kuifuatilia rekodi yake na kujua namna gani anaweza kumudu mazingira yetu.

Namna pekee ya kumpata kocha bora ni kufanya utafiti mzuri tena wa kina na kutumia jopo la wataalamu kumchunguza huyo ambaye mnahitaji.


PATRICK Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa uwezo wa wachezaji wa Simba unaongezeka kila siku hivyo anaamini wataleta ushindani msimu ujao.

Simba imeweka kambi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu pamoja na michuano ya kimataifa.

"Wachezaji wapo vizuri na wanaendelea vizuri hivyo imani yangu ni kuona kila mmoja anafanya kile ambacho nimemuelekeza.

"Ugumu mkubwa upo msimu ujao hasa ukizingatia ratiba imebana kuliko kawaida nasi tunapaswa tufanye vizuri pia," amesema.

Simba inatarajia kurejea Bongo Julai 31 baada ya kumaliza maandalizi yao ambayo yatatumia wiki mbili.



MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi ameunga mkono mfumo wa Klabu Maarufu ya Mchezo wa soka ya Yanga kuanzisha miradi ya kujitegemea katika azma ya kuiondoshea na utegemezi Klabu hiyo.

Balozi Seif Ali Iddi ameyasema hayo ofisini kwake Vuga-Zanzibar wakati akizungumza na Uongozi wa Yanga.

Balozi Seif amesema kwa kuwa Klabu hiyo ina dhamira sahihi ya kuendeleza Wachezaji wake katika azma njema ya kuimarisha ustawi wao yeye binafsi pamoja na Serikali iko tayari kusaidia nguvu zake ili kuona malengo iliyojipangia yanafanikiwa vizuri.


 Mwenyekiti wa Yanga Dr. Mshindo Msolla amemueleza Balozi Seif kwamba uongozi umelenga kuyasimamia mambo matano makubwa yatakayosaidia kuipeleka klabu hiyo katika mafanikio.

Mambo hayo ni pamoja na kuleta umoja katika kuipeleka timu kwa wanachama, kuimarisha Miradi iliyopo klabuni na kubuni mengine mipya, uwajibikaji na utawala bora pamoja na kuiendeleza miradi iliyopo Visiwani Zanzibar.

Amesema katika mfumo huo Mpya utakaoanzishwa, Wanachama watakuwa na uwezo wa kujua mapato na matumizi ya klabu kupitia mtandao wa kisasa wa Habari na Mawasiliano utakaokwenda sambamba na kuongeza Wanachama kutoka 17,000 hadi kufikia Milioni 1,000,000.

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.