Home
Unlabelled
YANGA YAZIPIGIA HESABU POINTI ZA RUVU SHOOTING
CEDRICK Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa wanahitaji kushinda kwenye mchezo wa leo dhidi ya Ruvu Shooting ili kuweza kupata pointi tatu muhimu.
Vinara hao wa ligi wenye pointi 55 wanatarajiwa kushuka uwanjani leo kusaka pointi tatu kama ambazo zinasakwa na Ruvu Shooting saa 10:00 jioni,
Kaze ameweka wazi kwamba mchezo wa leo utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na wapinzani wao kuhitaji kuweza kutibua rekodi yao ya kutokufungwa.
“Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu hasa ukizingatia kwamba wapinzani wetu wanahitaji kushinda kama ambavyo sisi tunahitaji lakini tumejiandaa katika hilo na tunahitaji ushindi.
“Wachezaji wapo tayari na wanajua kwamba kazi ipo kwenye kusaka ushindi hivyo hakuna ambacho tunahofia kwa sasa tupo tayari na tutafanya vizuri,”.
Kwenye msimamo Yanga ina pointi 55 baada ya kucheza mechi 21 kwa msimu wa 2021/22 haijapoteza mchezo kwenye mechi zote ilizocheza watashuka katika Uwanja wa Lake Tanganyika kusaka pointi tatu.
Post a Comment