ALIYEWAHI kuwa Kocha Mkuu wa Yanga ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soka la Vijana, Mkongomani, Mwinyi Zahera, amefunga mjadala wa ubora wa mshambuliaji Fiston Mayele na beki wa Simba, Henock Inonga.

Hiyo ni baada ya wachezaji hao kuzua mjadala mara baada ya mchezo wa Kariakoo Dabi uliozikutanisha Yanga dhidi ya Simba ambao ulichezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Ilikuwa ni Aprili 30,2022 wababe hao walikuwa kwenye msako wa pointi tatu,kwenye mchezo wa mzunguko wa pili.

Katika mchezo huo uliomalizika kwa suluhu, Inonga alifanikiwa kumzuia mshambuliaji huyo ambaye ni kinara wa mabao Ligi Kuu Bara akifunga 12.

 Zahera amesema katika mchezo huo, kila mmoja aliifanya kazi yake ipasavyo, lakini Inonga akafanikiwa kuzuia mashambulizi.

“Yanga haimtegemei mchezaji mmoja katika kufunga, kama ilivyokuwa kwa mabeki wa Simba wenyewe waliingia uwanjani kwa ajili ya kumkaba Mayele.

“Wenyewe waliamini Mayele ni mchezaji pekee angewafunga, katika mchezo huo baadhi ya wachezaji wa Yanga walishindwa kutumia nafasi za kufunga ambao walikuwa katika nafasi nzuri.

“Nipongeze viwango bora walivyokuwa navyo Mayele na Inonga ambaye yeye alijitahidi kufanya kazi yake vizuri ya kuzuia mashambulizi.”

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.