NAMUNGO FC YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA SIMBA LINDI
WENYEJI, Namungo FC wamelazimishwa sare ya 2-2 na mabingwa watetezi, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
Mabao ya Namungo ambayo mara mbili ilitangulia dhidi ya wazoefu wa Robo Fainali ya michuano ya klabu Afrika yamefungwa na Jacob Masawe dakika ya nane na Mzambia Obrey Chirwa dakika ya 54, wakati ya Simba yamefungwa na Shomari Kapombe dakika ya 42 na Kibu Dennis dakika ya 79.
Namungo wanafikisha pointi 30 katika mchezo wa 32, ingawa wanabaki nafasi ya tatu wakizidiwa pointi 13 na Simba ambao imecheza mechi ya 21 leo sawa na watani wao, Yanga wanaoongiza Ligi kwa pointi zao 55.
Post a Comment