May 2022

 


MTENDAJI Mkuu wa Klabu ya Simba Barbara Gonzalez na Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga Haji Manara leo wametinga katika Ofisi za Shirikisho la Mpira Tanzania, (TFF) ambapo waliiitwa kwa ajili ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya TFF.

Kila mmoja kwa nyakati tofauti kaweka wazi kwamba hakuna jambo ambalo wanaweza kuzungumza mpaka pale taarifa itakapotolewa.

Baada ya kutoka kuhojiwa na Kamati ya Maadili, CEO Barbara alisema hawezi kuongea chochote kwani wenye mamlaka ya kutoa tamko ni TFF.

Naye Haji Manara kwa upande wake amesema hawezi kuzungumza jambo lolote zaidi y kuawaachia wenye mamlaka kwa kuwa ni kesi.

“Hii ni kesi sasa mimi siwezi kuzungumza jambo lolote kuhusu hili na hakuna ugomvi sisi tulikuwa tunazungumza masuala yanayotuhusu,”.

Barbara aliandikiwa barua ya kufika katika Ofisi za TFF akiwa na tuhuma ya kufanya mahojiano na Chombo cha Habari cha nchini Afrika Kusini na kutamka baadhi ya maneno ambayo yanasemekana kuwa na ukakasi wa kuichafua Nchi, Klabu ya Yanga pamoja na Mpira wa Miguu wa Tanzania kwa ujumla.

Kwa upande wake Haji Manara sababu ya wito wake imeelezwa kuwa ni maandishi ambayo alichapishwa kwenye mtandao wake wa kijamii kuhusu Simba.

 

LEO Mei 20,2022 Kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa ametangaza orodha ya wachezaji wa timu hiyo watakaoingia kambini.

Wachezaji hao ambao wameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars ambacho kitaingia kambini kujiandaa na michezo ya kufuzu AFCON 2023 wana kazi ya kusaka ushindi kwenye mechi mbili za awali.

Kwa upande wa nyota ambao wametoka Simba ni sita wameitwa ikiwa ni pamoja na:-

 Aishi Manula

 Shomari Kapombe

 Mohamed Hussein

 Kennedy Juma

 Mzamiru Yassin

 Kibu Denis

 

 PABLO Franco,Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa tatizo ambalo linamsumbua kwa sasa ni ubora wa wachezaji wake hasa kwenye safu ya ushambuliaji.

Kwenye mchezo wao mzunguko wa pili dhidi ya Azam FC Uwanja wa Azam Complex uliochezwa Mei 18, mabingwa hao watetezi walilazimisha sare ya kufungana bao 1-1.

Ni Rodgers Kola alifunga dk ya 37 kwa upande wa Azam FC kisha lile la Simba lilifungwa na John Bocco na kufanya kwenye msako wa pointi tatu wagawane pointi mojamoja.

Pablo amesema:”Tumekuwa kwenye mwendo ambao hatujaupenda na tulipata nafasi mbele ya Azam FC lakini tumekwama kuzitumia hili ni tatizo.

“Ubora wa safu ya ushambuliaji kutoweza kutumia nafasi ambazo tumezitengeneza ni sababu ya kushindwa kupata matokeo, kwa hili tutalifanyia kazi kwa mechi zijazo,”

 Simba inafikisha pointi 50 ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo huku Azam FC ikiwa na pointi 33 nafasi ya 5 kwenye msimamo.

 

 MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa walistahili kupata ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Newcastel United.

Arsenal ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle United kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa St James Park.

Kichapo hicho kimeifanya timu hiyo kuwa kwenye wakati mgumu katika kusaka nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiwania nafasi hiyo na Tottenham.

Arteta anasema :”Ilikuwa ngumu sana. Kikawaida siwezi kukaa hapa na kuanza kuwatetea wachezaji kwa walichofanya uwanjani sio rahisi.

“Siku zote nimekuwa nikiwatetea lakini hapana sasa inatosha,wapinzani wetu walikuwa bora kwetu na tangu mchezo unaanza mpaka unakamilika likuwa ngumu kukubali kwani mambo mengine huwa yanakuwa hivyo,”.

 

BAADA ya kuwepo kwa tetesi kwamba Al Ahly ina mpango wa kumtoa kwa mkopo winga wake, Luís Miquissone, inaelezwa kwamba, uongozi wa Simba fasta umemfuata mchezaji huyo kutaka kumrejesha kikosini hapo.

Luis ambaye alikuwa mchezaji wa Simba kwa kipindi cha msimu mmoja na nusu kuanzia Januari 2020 hadi Agosti, 2021, tangu ajiunge na Al Ahly amekuwa hana nafasi kubwa ya kucheza chini ya Kocha Pitso Mosimane.

Winga huyo raia wa Msumbiji, anapata upinzani mkubwa kutoka kwa Percy Tau raia wa Afrika Kusini ambaye ndiye mchezaji anayetegemewa eneo la winga.

Akizungumza na Spoti Xtra moja kwa moja kutoka nchini Mali, meneja wa winga huyo, Djibril Cante, amethibitisha juu ya Simba kuwa katika mazungumzo na uongozi wa Al Ahly kuhitaji kumchukua Luis kwa mkopo.

“Ni kweli uongozi wa Simba unafanya mazungumzo juu ya kumpata Luis Miquissone kwa mkopo ili arejee tena ndani ya kikosi chao, mazungumzo yanafanywa kwa pande zote mbili za uongozi wa timu na uongozi wa mchezaji.

“Hakuna muafaka uliopatikana mpaka sasa, lakini bado mazungumzo yanaendelea, uongozi wa Al Ahly upo tayari kumtoa Luis kwa mkopo kutokana na kushindwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara,” alisema kiongozi huyo.

Kwa upande wa Simba, Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally, alisema: “Masuala ya usajili kwa sasa hatupo tayari kuyazungumzia, tupo kwenye maandalizi ya mechi zilizosalia za ligi na nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Yanga, muda wa usajili ukifika kila kitu kitajulikana.”

 

 MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Geita Gold v  Simba unaotarajiwa kuchezwa Mei 22,2022 utachezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Geita Gold imekuwa kwenye mwendo mzuri msimu huu baada ya kuanza kwa kusausua mwanzoni mwa msimu na sasa inacheza soka bora.

Mchezo wake uliopita ilicheza dhidi ya Mbeya Kwanza na ilishinda bao 1-0 Uwanja wa Majimaji,Songea.

 


WENYEJI,  Namungo FC wamelazimishwa sare ya 2-2 na mabingwa watetezi, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ilulu mjini Lindi. 
Mabao ya Namungo ambayo mara mbili ilitangulia dhidi ya wazoefu wa Robo Fainali ya michuano ya klabu Afrika yamefungwa na Jacob Masawe dakika ya nane na Mzambia Obrey Chirwa dakika ya 54, wakati ya Simba yamefungwa na Shomari Kapombe dakika ya 42 na Kibu Dennis dakika ya 79.
Namungo wanafikisha pointi 30 katika mchezo wa 32, ingawa wanabaki nafasi ya tatu wakizidiwa pointi 13 na Simba ambao imecheza mechi ya 21 leo sawa na watani wao, Yanga wanaoongiza Ligi kwa pointi zao 55.

 

CEDRICK Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa wanahitaji kushinda kwenye mchezo wa leo dhidi ya Ruvu Shooting ili kuweza kupata pointi tatu muhimu.

Vinara hao wa ligi wenye pointi 55 wanatarajiwa kushuka uwanjani leo kusaka pointi tatu kama ambazo zinasakwa na Ruvu Shooting saa 10:00 jioni,

Kaze ameweka wazi kwamba mchezo wa leo utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na wapinzani wao kuhitaji kuweza kutibua rekodi yao ya kutokufungwa.

“Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu hasa ukizingatia kwamba wapinzani wetu wanahitaji kushinda kama ambavyo sisi tunahitaji lakini tumejiandaa katika hilo na tunahitaji ushindi.

“Wachezaji wapo tayari na wanajua kwamba kazi ipo kwenye kusaka ushindi hivyo hakuna ambacho tunahofia kwa sasa tupo tayari na tutafanya vizuri,”.

Kwenye msimamo Yanga ina pointi 55 baada ya kucheza mechi 21 kwa msimu wa 2021/22 haijapoteza mchezo kwenye mechi zote ilizocheza watashuka katika Uwanja wa Lake Tanganyika kusaka pointi tatu.

 

ALIYEWAHI kuwa Kocha Mkuu wa Yanga ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soka la Vijana, Mkongomani, Mwinyi Zahera, amefunga mjadala wa ubora wa mshambuliaji Fiston Mayele na beki wa Simba, Henock Inonga.

Hiyo ni baada ya wachezaji hao kuzua mjadala mara baada ya mchezo wa Kariakoo Dabi uliozikutanisha Yanga dhidi ya Simba ambao ulichezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Ilikuwa ni Aprili 30,2022 wababe hao walikuwa kwenye msako wa pointi tatu,kwenye mchezo wa mzunguko wa pili.

Katika mchezo huo uliomalizika kwa suluhu, Inonga alifanikiwa kumzuia mshambuliaji huyo ambaye ni kinara wa mabao Ligi Kuu Bara akifunga 12.

 Zahera amesema katika mchezo huo, kila mmoja aliifanya kazi yake ipasavyo, lakini Inonga akafanikiwa kuzuia mashambulizi.

“Yanga haimtegemei mchezaji mmoja katika kufunga, kama ilivyokuwa kwa mabeki wa Simba wenyewe waliingia uwanjani kwa ajili ya kumkaba Mayele.

“Wenyewe waliamini Mayele ni mchezaji pekee angewafunga, katika mchezo huo baadhi ya wachezaji wa Yanga walishindwa kutumia nafasi za kufunga ambao walikuwa katika nafasi nzuri.

“Nipongeze viwango bora walivyokuwa navyo Mayele na Inonga ambaye yeye alijitahidi kufanya kazi yake vizuri ya kuzuia mashambulizi.”

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.