BAADA ya kuongoza kikosi cha Simba kwenye mechi mbili za ligi na kushinda zote, Zoran Maki, Kocha Mkuu wa Simba anatarajiwa kukiongoza kikosi hicho kwenye mechi za kimataifa za kirafiki ambapo wanatarajia kucheza na Asante Kotoko ya Ghana.
Ni kwenye mashindan maalumu ambayo Simba wamealikwa yanatarajiwa kufanyika nchini Sudan wakialikwa na Klabu ya Al Hilal.
Jumatano ama Alhamisi vinara hao wa ligi wenye pointi sita wanatarajia kuondoka nchini Tanzania kuelekea kwenye mashindano hayo.
Ratiba ambayo imetolewa inaonyesha kwamba Agosti 28 watacheza mchezo wa kimataifa dhidi ya Asante Kotoko kisha Agosti 31 watacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Al Hilal kisha kete ya tatu itakuwa ni Septemba 3,2022 dhidi ya AS Arta Solar.
Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa ni heshima kwa Simba kualikwa kwenye mashindano hayo.
“Ni heshima kwetu kualikwa kwenye mashindano maalumu ambayo yanafanyika na hii inatokana na mahusiano mazuri na timu nyingine,”